Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga linachunguza tukio linalomhusisha mwanaume mmoja kwa tuhuma za
kuwalawiti watoto wake wawili wanafunzi wa shule ya msingi Mapinduzi B, iliyopo
kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi
amethibitisha mwanaume huyo kukamatwa kwa ajili ya uchunguzi.
Kamanda Magomi amesema
upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua
zaidi za kisheria.
Akizungumzia tukio hilo
kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Kambi
Butete amesema Februari 22 Mwaka huu majira ya saa tano asubuhi watoto hao
walifikishwa katika Hospitali hiyo na kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari ambapo
majibu ya vipimo vyao yamekabidhiwa kwa vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua
za kisheria.
Misalaba Blog imezungumza
na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Mapinduzi B, Hassan Hemed ambaye ameeleza namna alivyopokea taarifa za tukio
hilo, na kusema kuwa kushamiri kwa matukio hayo inachangiwa na wazazi na walezi
kutowajibikia jukumu la malezi bora na makuzi kwa watoto.
‘Hizi
taarifa za hawa watoto wawili nilizipokea kwa kuletewa na watu ambao wao
wanasema ni wana harakati ndiyo waliniletea hawa watoto saa sita usiku asubuhi
nikaenda kwa hawa watoto mpaka wanapoishi mpaka ndani kwako bi kweli wanalala
chumba kimoja na baba yao mzazi’.amesema Mwalimu Hemed
Taarifa za kulawitiwa kwa
watoto hao ziliripotiwa kwa Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mapinduzi B, usiku
wa Februari 22, Mwaka huu 2023.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Social Plugin