Na Mapuli Kitina Misalaba
Viongozi wa Dini mkoani Shinyanga wametoa tamko maalum wakiiasa jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la upigaji kura ifikapo Oktoba 29, 2025, ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo kuanzia ngazi ya kata.
Wakizungumza kwa umoja wao kupitia Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) Mkoa wa Shinyanga, viongozi hao wameazimia kuiunga mkono serikali katika kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura kwa amani, utulivu na umoja, wakisisitiza kuwa uchaguzi ni sehemu muhimu ya demokrasia na si sababu ya kuvuruga amani.
Akisoma tamko hilo kwa niaba ya viongozi wa Dini, Askofu Mstaafu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Joseph Makala, amesema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha nchi inabaki salama, kwani amani ni tunu na msingi wa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake, Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amewahimiza viongozi wa Dini, machifu na wazee wa kimila kuendelea kuliombea taifa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, akisisitiza kuwa maombi yana mchango mkubwa katika kudumisha utulivu wa taifa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amewahakikishia wananchi kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha siku ya kupiga kura inafanyika kwa usalama na utulivu wa hali ya juu, akiwataka wananchi kujitokeza bila hofu kutumia haki yao ya kikatiba.
Viongozi hao wa Dini wametoa wito kwa jamii kuendelea kudumisha upendo, mshikamano na kuheshimu maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakisisitiza kuwa amani ni zawadi ambayo kila raia ana wajibu wa kuilinda.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza kwenye hafla hiyo leo Oktoba 18, 2025.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza kwenye hafla hiyo leo Oktoba 18, 2025.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, akizungumza kwenye hafla hiyo leo Oktoba 18, 2025 Mkoani Shinyanga.

Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) Mkoa wa Shinyanga Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala, akizungumza leo Oktoba 18, 2025.

Social Plugin