Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watu tisa wanaosadikiwa kuhusika katika tukio la ujambazi lililotokea Februari 4, 2023 katika kambi ya Wachina wanaojenga reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR eneo la Old-Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga.
Katika
taarifa yake kwa Vyombo vya Habari leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi hilo
limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kufuatia msako na doria zilizofanyika
katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamanda
Magomi amesemna pamoja na watuhumiwa hao jeshi hilo limekamata pesa za kigeni
za nchi mbalimbali ambapo amesema uchunguzi unaendelea na kwamba watuhumiwa
watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Kamanda
Magomi ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutojihusisha na
hujuma dhidi ya mradi wa reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR pamoja na uhalifu
mwingine.
Kamnada
huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga amesema kuhujumu miundombinu katika
mradi wa SGR na miradi mingine ni kurudisha nyuma juhudi za serikali ambayo
imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.
Social Plugin