Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti wa vijana wakatoliki wafanyakazi VIWAWA kanda ya ziwa Baraka Shilolelo amewakumbusha viongozi Chama hicho cha kitume majimbo pamoja na walezi ngazi ya kanda kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano uliopo, ikiwa ni pamoja na kutekeleza utume huo kwa maslahi ya kanisa.
Ameyasema hayo kwenye kikao cha mwanzo wa Mwaka 2023 cha viongozi mbalimbali wa VIWAWA na walezi wa majimbo kanda ya ziwa ambacho hufanyika mara mbili kwa Mwaka kwa lengo la kujadili dira ya Mwaka pamoja na utekelezaji wa maazimio ya VIWAWA Taifa..
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa vijana center Mjini Shinyanga ambapo Shilolelo amewasisitiza viongozi hao kuendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali ili kutekeleza utume huo kwa ajili ya manufaa ya kanisa.
“Niwasihi viongozi wenzagu tusiwasaidie vijana tunaowaongoza kulalamika tuwape majibu sahihi ya maswali yao viongozi sahihi ni wale wanaotoa majibu ya wale wanaowaongoza kwahiyo nawaomba sana tusitangulize misimamo yetu tutangulize maslahi ya wale tunaowaongoza tupendane, tuheshimiane, tusaidiane lakini tuhurumiane pia maana kila kitu tunachokifanya nikwa ajili ya kristo kusaidiana kuwe ni sehemu ya maisha yetu lakini ushirikiano utatufikisha kwa kristo kama matarajio yetu”.amesema Mwenyekiti Shilolelo
Katika kikao hicho viongozi na walezi wa VIWAWA kutoka majimbo mbalimbali ya kanda wametoa ushauri wao ikiwemo wazo la kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kuendelea kulijenga Kanisa.
Viongozi wa VIWAWA kanda ya Ziwa wamekaa kikao cha Mwanzo wa Mwaka kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Mkutano utakaofanyika mwezi April Mwaka huu pamoja na kongamano la kanda litakalofanyika mwezi June Mwaka huu 2023.Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa VIWAWA kutoka majimbo mbalimbali ikiwemo jimbo katoliki la Shinyanga, jimbo katoliki la Musoma, jimbo katoliki la Rulenge Ngara, jimbo katoliki la Geita pamoja na viongozi kutoka jimbo kuu katoliki la Mwanza.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Padre Emmanuel Lyanga mlezi wa VIWAWA kanda ya Ziwa, Padre Peter Mkunya Lyuba mlezi wa VIWAWA jimbo la Shinyanga, Padre Pamphilius Kitondo John mlezi wa VIWAWA jimbo la Rulenge Ngara, makamu Mwenyekiti kanda ya Ziwa Gerald Charles Msoke, katibu wa VIWAWA kanda ya Ziwa John Robert Melli, katibu msaidizi VIWAWA kanda ya Ziwa Suzana Daud, mhasibu VIWAWA kanda ya Ziwa Steve Simon Mlioo, Mwenyekiti VIWAWA jimbo katoliki la Geita Musa Masolwa, Mwenyekiti VIWAWA jimbo katoliki la Shinyanga Leonard Mapolu,Mwengine ni katibu VIWAWA jimbo katoliki la Geita Stephano Magibo, katibu VIWAWA jimbo katoliki la Musoma Dominiko Sheki, Mwenyekiti VIWAWA jimbo katoliki la Mwanza Raphael Joseph pamoja na katibu msaidizi VIWAWA jimbo katoliki la Rulenge Ngara Adera Fabiani.
Social Plugin