Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mkuu wa jeshi la polisi
kitengo cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Mrakibu msaidizi wa
Polisi Debora Lukololo amewataka
watumiaji wa vyombo vya moto pamoja na watembea kwa miguu kushiriki kikamilifu
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama.
Amesema jeshi hilo katika
wiki ya nenda kwa usalama barabarani pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika
litatoa elimu ya usalama barabarani, ukaguzi wa vyombo vya moto na ukaguzi wa leseni.
Amewataka wananchi
kutumia fursa hiyo ili kuzijua sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani
ili kuepukana na ajali barabarani
Wakati huo huo mrakibu
msaidizi wa Polisi Debora Lukololo amekemea kitendo cha kuhujumu miundombinu ya
barabarani ikiwemo alama za usalama barabarani kwani kitendo hicho ni kinyume
cha sheria za Nchi.
Machi 13 hadi 17 Mwaka
huu 2023 Mkoa wa Shinyanga utaadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani na
kwamba kauli mbio ya Mwaka huu 2023 inasema ‘TANZANIA BILA AJALI INAWEZAKENA
TIMIZA WAJIBU WAKO’
Social Plugin