Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wazazi na walezi wa wanafunzi
katika shule ya msingi Mwadui kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
wamekumbusha kutimiza wajibu wao kwa watoto ikiwemo malezi bora pamoja na kufuatilia
maendeleo ya wanafunzi shuleni.
Wito huo umetolewa na Mwalimu
mkuu msaidizi wa shule ya msingi Mwadui, Twaha Rashid wakati akizungumza na
Misalaba Blog ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wazazi kuwajibika ipasavyo suala
la malezi ili kukomesha vitendo viovu vinavyochangiwa na mmomonyoko wa maadili.
Mwalimu Rashid amesema jamii
inawajibu mkubwa wa kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa kushirikiana na
uongozi wa shule pamoja na serikali za mitaa ili kumlinda mtoto.
Mwalimu Rashid amewaomba
wazazi na walezi kuwa mfano kwa watoto wao na kwamba wanapaswa kuishi maisha
ambayo yatamjenga na kumuimarisha mtoto katika maisha ya kila siku.
Social Plugin