Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na walengwa wa kaya maskini
unaotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, wameendelea na zoezi la
kupanda miti ikiwa ni hatua ya kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi
zoezi hilo
leo limefanyika katika Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ambapo
takribani miche ya miti 1200 imepandwa katika eneo lililopo karibu na ofisi ya
serikali ya mtaa huo.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Afisa Maliasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana
Ezra Manjerenga amesema zoezi hilo linatekelezwa chini ya Mradi wa TASAF kwa ajili
ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Tunaendelea na juhudi zetu kubwa
za kutekeleza kampeni ya usimamizi wa mazingira na kwa Manispaa ya Shinyanga
tunakampeni inaitwa ‘MTU NA MTI’ lakini vilevile tunatekeleza maagizo ya kila
Halmashauri kupanda miti Milion moja na laki tano Shinyanga toka kipindi cha
nyuma kwa historia sisi ni wahanga wa mabadiliko ya tabianchi”.amesema afisa mazingira Manjerenga
“Katika mradi tulionao huu hapa
mtaa wa Dome tumepanda miti 1200 na hii inagusa lengo letu la Halmashauri
ambapo tunaenda kufikia asilimia 86 sasa ya utekelezaji wa agizo la serikali
kwa kila Halmashauri kupanda miti Milion moja na laki tano”.amesema Afisa mazingira Manjerenga
Manjerenga amesema mbali
na mafanikio yaliyopo kupitia lakini pia zoezi hilo limekuwa likikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ufugaji holela hali inayosababisha uharibifu wa
miti iliyopandwa.
Aidha Afisa Mazingira Manjerenga amewaomba wakazi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi kufuata miche ya miti inayotolewa
bure katika ofisi hiyo ili kupendezesha mazingira.
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa amesema atahakikisha mradi huo anausimamia ipasavyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Katika zoezi hilo Mzabuni
na mshauri wa kamati ya TASAF mtaa wa Dome Joseph Kisanko amesema kuwa lengo la
mradi huo ni kuboresha mazingira.
Nao baadhi ya walengwa wa
TASAF ambao wanatekeleza mradi huo wa upandaji miti wamesema pamoja na faida
nyingine lakini pia kupitia mradi huo wanajikwamua kiuchumi kupitia ujira
wanaolipwa
Shughuli hiyo
imehudhuriwa na wananchi, wadau, viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa
chama ambapo nao wamesisitiza juu ya ushirikiano katika kutunza mazingira.
Afisa Mariasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga akitoa elimu kuhusu namna bora ya upandaji wa miti.
Afisa Mariasili na Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga akitoa elimu kuhusu namna bora ya upandaji wa miti.
Upande wa kushoto ni Mzabuni na mshauri wa kamati ya TASAF mtaa wa Dome Joseph Joaster Kasanko na upande wa kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa wakishiriki katika zoezi la kupanda miti.
Upande wa kushoto ni Mzabuni na mshauri wa kamati ya TASAF mtaa wa Dome Joseph Joaster Kasanko na upande wa kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa wakishiriki katika zoezi la kupanda miti.
Social Plugin