Kamati ya siasa ya chama cha
mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Februari 17, 2023 imefanya ziara ya kutembelea na
kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoondelea kutekelezwa katika Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga ikiwemo ujenzi wa soko kuu la kisasa mjini Shinyanga.
Akizungumza Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe ametumia nafasi hiyo kupongeza juhudi
mbalimbali zinazofanywa na serikali katika utatuzi wa changamoto za wananchi
Manispaa ya Shinyanga.
“Niipongeze
Manispaa yetu ya Shinyanga chini ya Mstahiki Meya lakini pia na Mkurugenzi wetu
na wataalam wetu kwa juhudi za maksudi zinazofanywa tunauona mji wetu
unavyobadilika na tunaamini kabisa kwamba unaenda kutuongezea hadhi badaye”.amesema
Mwenyekiti Makombe
Katika ziara hiyo Misalaba Blog imezungumza na mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga Mh. Johari Samizi ambaye amewasisitiza wataalam na wakuu wa
idara wa Halmashauri ya Manispaa
wanaosimamia miradi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili wananchi
waweze kunufaika.
DC Samizi amewaomba wananchi
wa Wilaya ya Shinyanga kuendelaa kuunga mkono juhudi za serikali ambapo amesema
atasimamia kuhakikisha miradi inawanufaisha wananchi kama mpango wa serikali
chini ya ilani za chama cha mapinduzi CCM.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Mh. Johari Samizi ametumia nafasi hiyo kuendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi kwa
lengo la kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Wilaya hiyo ya Shinyanga.
Misalaba Blog pia imezungumza
na katibu wa itikadi, siasa na uenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana
Said Bwanga ambaye ametaja baadhi ya
maeneo ambayo kamati ya siasa
imetembelea na kukagua huku akitaja maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo.
“Katika
ziara yetu tumetembelea shule ya wasichana iliyopo Butengwa kata ya Ndembezi
katika shule hiyo tumeona maendeleo yanakwenda vizuri na mpaka sasa hatua
iliyofikiwa ni hatua kubwa tumeambia ni takribani asilimia 80 vilevile tumeweza
kutembelea zahanati ya Seseko na ujenzi wa barabara ya Seseko kwa kweli serikali
hii inayoongozwa na Rais mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan wanafanya vizuri
daraja la Ndembezi limejengwa vizuri tena kwa kiwango wa juu”.
“Tumetembelea
daraja la Old Shinyanga nalo uongozi wa Manispaa ya Shinyanga wameliboresha
vizuri hakuna kero tena kwa wananchi tulipotoka pale tumetembelea mradi wa maji
kata ya Chibe kwa kweli tumeona mradi unaendelea vizuri, tumetembelea ujenzi wa
kituo cha Afya Kambarage hatujabaini changamoto”.amesema
Bwanga
“Kamati
ya siasa tumeweza kutembelea ujenzi wa soko la wamachinga lililopo Ngokolo
ambapo tumeomba mnada unaofanyika Jumamosi tu uwe unafanyika siku mbili
Jumamosi na Jumapili lakini pia wawekewe taa ili wananchi waweze kufanyakazi
mpaka usiku lakini tumeenda kutembelea soko kuu la mjini tumeona ujenzi
unaendelea vizuri”.
“Kamati
ya siasa pia tumetembelea eneo la Lubaga katika ujenzi wa barabara inayotokea
Lubaga kuelekea Old Shinyanga pamoja na kwamba mkandarasi alikuwa amepewa miezi
kumi awe amemaliza ambayo bado haijaisha lakini katika vile vifusi imekuwa ni
kero na changamoto kwa wananchi wa Shinyanga mara nyingi ajali zinatokea pale
kwahiyo chama cha mapinduzi kimetoa maagizo mkandarasi kuanzi sasa awe
anamwagia maji katika maeneo hayo kuzuia vumbi wakati wakiendelea na ukarabati
wakati huo huo tumewaagiza wakamilishe haraka tuta lililopo barabarani lisije
kuleta ajali”.amesema Katibu Mwenezi Bwanga
Kwa upande wake Mbunge wa
jimbo la Shinyanga Mjini Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi,vijana,
ajira na wenye ulemavu,Paschal Patrobas amesema
hatua mbalimbali za uboreshaji wa masoko zinaendelea vizuri katika jimbo hilo.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Ndembezi, Old Shinyanga, Chibe, Kambarage, Ngokolo pamoja na kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni hatua ya kusimamia ilani ya chama hicho.
Social Plugin