MSIGWA ATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA SHERIA ZA NCHI, TAASISI YA WAANDISHI WA HABARI MTANDAONI (TOMA) YAZINDULIWA RASMI.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waandishi wa habari za mtandaoni Nchini wametakiwa kuzingaia sheria zilizopo katika sekta hiyo na kwamba wanapaswa  kuandika habari zenye kuleta matokeo chanya kwa wananchi na serikali kwa jumla.

Hayo yamezungumza na mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo na msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa akiwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance) TOMA iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwl. Julius Nyerere uliopo katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Hafla hiyo imeratibiwa na chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT ambapo Msingwa amewasisitiza waandishi hao kuzingatia maadili yao.

Mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo na msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa akiwa amemwakilishi waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Mh. Nape Nnauye, ametumia nafasi hiyo kuwataka waandishi wa habari za mtandaoni kuandika habari kwa weledi na kuepuka habari za upotoshaji ambazo huzua taharuki na huchochea mgogoro Nchini.

Tasnia ya habari iko mikononi mwa vyombo vya habari mtandaoni, twendeni tukaoneshe weledi wa hali ya juu hicho ndicho kitakachotufanya tuaminike na jamii lakini pia ni lazima tuangalie maadili ya uandishi wa habari yanasema nini, ni lazima tuangalie sheria za Nchi yetu zinasema nini hatuwezi kuwa waandishi wa habari za mtandaoni kwa kujikita tu kwenye kuzua taharuki, kuvunja sheria au kuchonganisha jamii na jamii au jamii na serikali”.amesema Msigwa

“Tumetoka tulipotoka vyombo vya habari vikimilikiwa na wanasiasa na wafanyabiashara, akija mmiliki anasema weka hiki usiweke hiki. Tuacheni kutumika, hapo ndipo heshima yetu itakuwepo, fanya kazi yako kwa weledi”.amesema Msigwa

Aidha Msigwa amewasisitiza waandishi wa habari wenye elimu ya chini kujiendeleza ili kuimarika zaidi huku akipongeza juhudi za chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) kwa kuanzisha wazo hilo ambapo itasaidia waandishi wa habari za mtandaoni waweze kuwa na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Katika taarifa yake Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha Bwana Claud Gwandu amesema TOMA imeanzishwa baada ya chama hicho  APC kumaliza mradi waliokuwa wakitekeleza wenye lengo la kusaidia waandishi wa habari za mtandaoni ambao walikuwa na changamoto mbalimbali za kitaaluma ambapo mafunzo ya aina mbalimbali yalitolewa ili kuwaimarisha na kupunguza tatizo la ajira kwa waandishi wa habari.

“Toma imesajiliwa rasmi Mwaka jana 2022 baada ya mradi uliokuwa unaendeshwa na Arusha Press Club (APC) kwa kushirikiana na Freedom House pamoja na PACT mradi huu ulianza Mwaka 2018 na ulikuwa na malengo ya kuwasaidia waandishi wa habari za mtandaoni ambao walikuwa na changamoto mbalimbali za kitaaluma mwanzoni tulianza na waandishi wa habari za mtandaoni 23 kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Tanzania”. amesema Mwenyekiti wa APC Gwandu

“Katika utekelezaji wa mradi huo tulikuwa tukitoa mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo ya kiusalama kazini, mafunzo ya sheria za uandishi wa habari, mafunzo kuhusu maadili na kanuni za uandishi wa habari na mambo mengine mbalimbali”. amesema  Gwandu

“Baada ya kuelekeza kumaliza mradi huo tukaona kwamba kuna unaumuhimu wa kuanzisha chombo ambacho kitakuwa kinasimamia yale ambayo yalikuwa yanafanywa na Club ya waandishi wa habari  Mkoa wa Arusha  katika kutekeleza mradi na hiki chombo kiko wazi kwa waandishi wa habari wa Tanzania nzima wanaojihusisha na uandishi wa habari za mtandaoni ambao wanauhiari wa kujiunga na chombo hiki”.amesema Mwenyekiti wa APC Gwandu

Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo wamekipongeza chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha kwa kuanzisha wazo hilo ambapo wameahidi kuendeleza kushirikiana na TOMA huku wakiwaomba waandishi wa habari za mitandaoni kutumia fursa hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake makamu Mwenyekiti wa Tanzania Online Media Alliance (TOMA), Salome Kitomari amesema atahakikisha taasisi hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa taaluma huku akiwakumbusha waandishi wa habari kutumia fursa hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka maudhui mazuri.

Makamu Mwenyekiti wa TOMA ambaye nia ni Mwenyekiti taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) Salome Kitomari ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazofanya katika kuimarisha umoja wa Taifa huku akiishukuru serikali kwa kuweka uhuru wa vyombo vya habari.

Hafla ya uzinduzi wa taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance) TOMA imeratibiwa na chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa habari akiwemo Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation (TMF) Dastan Kamanzi, Mkurugenzi wa Freedom House Daniel Mahal Lema, Mwenyekiti taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA TANZANIA) Salome Kitomari, Mtaalam wa mambo ya habari kutoka ubalozi wa Marekani Japhet Sanga akiwa amemwakilisha kaimu mkurugenzi wa USAID, Bwana Bret Saalwaechter.

Wadau wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni pamoja na mwakilishi wa Legal and Human Rights Centre (LHRC) Hidaya Haonga, Mwakilishi wa Tanzania media coomen’s  Association (TAMWA) Bwana Godwin Assenga pamoja na Mwakilishi wa MISA TAN Tanzania Bwana Augustino Lucas.

Aidha waandishi wa habari kutoka katika vyombo vya habari  ikiwemo Blogs na Online Tv kutoka mikoa mbalimbali Nchini Tanzania wameshiriki uzinduzi huo wa taasisi huo  wa taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance) TOMA ambao umefanyika Ijumaa Februari 10,2023 na kwamba umeratibiwa na chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT.