WANAWAKE DOME SHINYANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wanawake wametakiwa kuchangamkia mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Halmashauri badala ya kuchukua mikopo kandamiza ambayo imekuwa ikiwasababishia migogoro na kufilisiwa mali.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Bwana Solomon Nalinga wakati akizungumza na Wanawake wa Mtaa huo kwenye kikao kilicholenga kubainisha fursa mbalimbali zilizopo kwa kundi hilo.

Bwana Nalinga amewaomba wanawake wa mtaa huo kujiunga kwenye vikundi  kama moja ya sifa na vigezo vya kupata mikopo inayotolewa na halmashauri kwa riba nafuu

Misalaba Blog imezungumza na baadhi ya wanawake wa mtaa wa Dome waliohudhuria kikao hicho ambapo wameahidi kuwa mabalozi waaminifu kwa wanawake wengine wanaojiunga kwenye vikundi kwa ajili ya kuchukua mikopo.