MWALIMU MKUU WA SHULE YA BUGOYI B – MJINI SHINYANGA AWAOMBA WAZAZI NA WALEZI KUCHANGA CHAKULA CHA WATOTO ILI KUONGEZA UFAULU

 
 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga 

Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Bugoyi A iliyopo Manispaa ya Shinyanga wamekumbushwa kuendelea kushiriki kikamilifu kutoa michango ya chakula shuleni kwaajili ya watoto wao. 

Wito huo umetolewa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bugoyi A, Mwalimu Alex Juma wakati akizungumza na Misalaba Blog ofisini kwake. 

 Amesema katika shule hiyo kunachangamoto ya baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kutoa michango hiyo ambayo ni muhimu kwa upatikanaji wa chakula cha watoto ili waweze kuhimili masomo yao. 

Katika hatua nyingine Mwalimu Alex ametaja moja ya umuhimu wa kupata chakula shuleni ikiwa ni kusaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika masomo yao.