Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wito umetolewa kwa waislam wote Wilaya ya Shinyanga kuishi matendo yanayompendeza Mwenyezi Mungu hasa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Wito huo umetolewa leo na Shekhe wa Wilaya ya Shinyanga Sudi Kategile wakati akizungumza na Misalaba Blog ilipomtembelea ofisini kwake.
Kategile amewataka waislam kutumia kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda matendo mema bila kubagua Dini wala kabila
Ametumia fursa hiyo kuwasisitiza waislam wote kutekeleza ibada ya funga katika kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Wakati huo huo Shekhe Kategile amewakumbusha waamini wa dini ya kiislam kuendelea kuomba Amani ya nchi ikiwa ni pamoja na kuombea viongozi wa serikali
Leo Waislam wameingia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa siku 30, ndani ya wiki nne zijazo ambapo mamilioni ya waislamu watajinyima kula na kunywa kuanzia mapema alfajiri
Social Plugin